Diwani ya Tamasha

Diwani ya Tamasha

November 9, 2023
Views: 18
Id: 15276
 • Report
  Report This Listing
  Login Required
 • Download
 • Print
 • Bookmark
 • Share
  Share This Listing
Media
Description:

Tajiriba ya miaka mingi ya kuandaa wanafunzi kwa mitihani ya kitaifa katika kiwango cha shule za upili imenifunza kuwa si wengi ambao hushabikia maswali ya ushairi katika mitihani.Wengi wamejazwa kasumba potofu kuwa ushairi ni utanzu mgumu.Jambo hili limeniatua moyo kwani kulingana nami,huu ndio utanzu mwepesi zaidi ambao kwao,mtahiniwa anaweza kukwangura alama za juu zaidi.Hii ndiyo imekuwa sababu kubwa ya kuandika kitabu hiki ili,japo kwa njia finyu,kichangie katika kuimarisha matokeo ya wanafunzi kwenye kitengo cha ushairi.

Aidha,baada ya kutunga mashairi na kuyatumia katika tamasha za drama na muziki kwa muda mrefu,nilihisi kuwa kazi hii ingetumiwa katika kufikia watu wengi zaidi kama ingetungiwa kitabu.Ni kwa misingi hii ndiposa nimependekeza kazi hii iitwe Diwani ya Tamasha.Kwangu,hii itakuwa heshima kubwa kwa wanafunzi wa Nyamagwa Boys ambao kwa miaka kumi na mitatu niliyokuwa nao,hamna mwaka hata mmoja ambao tulikosa kuwakilisha Mkoawa Nyanza katika tamasha za muziki – kiwango cha kitaifa.Isitoshe,kazi hii ni dhihirisho tosha kuwa kizaliwacho huwa kizuri zaidi kuliko kinachozaa.Shairi kwa anwani ukware lilitungwa na malenga mwendazake Hesborn Nyairo (Mungu amweke mahali pema) aliyeinukia kuwa mmoja kati ya wanafunzi wangu maarufu zaidi.Shairi hili liko katika diwani hii kama kumbukizi kwa heshima yake.

Katika kazi hii, imeonelewa kuwa ni bora kuangazia aina za maswali ambayo aghalabu hutokea katika mitihani ya kitaifa.Licha ya haya, maelezo mafupi kuhusu mambo muhimu yanayohitajika ili kulikabili barabara kila aina ya swali yametolewa.Baada ya kufanya haya yote, kuna mashairi yaliyotungiwa maswali mahsusi na majibu yao.Kwa njia hii ndogo, tunashawishika kuwa watahiniwa watanufaika pakubwa.

Contact Information
Price: ksh450.00
Categories:   
Phone: 0703204991
Address: santa plaza 1 floor,suit 101,Ngong road, Kilimani, Nairobi

Post New Review

Related Listings
Shedule a Test Drive
[dhvc_form id="2578"]
Apply For TradeIn With Us
[dhvc_form id="2578"]
Send Your Offer
Send Message
error: Content is protected !!